"Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke, kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba", (Mathayo 7:24 na 25).

Mtumishi wa Mungu David na Veronique Holland wote ni watumishi wa Mungu waliosimikwa ambao wanakaa katika nchi ya Ufaransa ya kusini Maono yao ya kubadilisha mataifa ni Kufundisha na kuhubiri neno la Mungu kwa usahihi, kiurahisi na kwa uwazi katika njia ambayo inaweza kutumiwa kivitendo katika maisha ya kila siku.

Wanafanya hivyo kupitia mikutano ya kimataifa na kozi kwa njia ya posta katika lugha ya kiingereza na kifaransa. Mtandao wenye lugha mbalimbali unafundisha mafundisho ya sauti ndani ya tovuti katika lugha ya kiingereza, lakini makala mbalimbali zinapatikana katika lugha zote duniani. Vitendea kazi vya huduma kama--vitabu, sidi, kanda za sauti, kozi za Biblia hizi zote zinapatikana katika tovuti yetu.